• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Maeneo ya Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Kilimo
    • Maeneo ya Madini
    • Maeneo ya Uwekezaji wa Mazingira
  • Huduma Zetu
    • Huduma Sekta ya Afya
    • Huduma Sekta ya Elimu
    • Huduma Sekta ya Maji
    • Huduma Sekta ya Mazingira
    • Huduma Sekta ya Maendeleo ya Jamii
    • Huduma Sekta ya Ardhi na Maliasili
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Huduma za Kijamii
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba Vikao vya Halmashauri
  • Miradi mbalimbali
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Mbalimbali
    • Taratibu
    • Gazeti la Serikali
    • Taarifa
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Video Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Habari Mpya

Wananchi wajenga madarasa manne Sekondari Gambajiga, DC Misungwi akabidhi mabati 108.

Imewekwa : December 11th, 2020

Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda  akabidhi mabati 108 yenye thamani ya shilingi  Milioni 2. 8 kwa ajili ya kupaua vyumba viwili  vya Madarasa ya Sekondari mpya yaliyojengwa na Wananchi katika Kijiji cha Gambajiga,  Wilayani Misungwi, Mkoani Mwanza.

Akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Gambajiga katika eneo la Ujenzi wa Sekondari hiyo, Juma Sweda amewataka  Wananchi hao kueezeka haraka madarasa hayo mawili  na kukamilisha na mengine ikiwemo  Jengo la Utawala na kuwahakikishia kwamba Shule hiyo mpya ya Sekondari inafunguliwa mwezi Januari mwaka 2021, ambapo amewaomba kuchapa kazi na kukamilisha ujenzi huo mapema ili Wanafunzi waanze kunufaika na kupata elimu karibu.

Juma Sweda amewapongeza Wananchi wa Kijiji cha Gamabajiga Kata ya Kanyelele kwa juhudi na kazi kubwa waliyoionyesha kwa kuanzisha ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari, lengo ikiwa ni kuongeza na kupandisha  kiwango cha Elimu katika Wilaya ya Misungwi na kuondoa adha kwa watoto kutembea umbali mrefu kwenda shule na Serikali itatoa Walimu mara baada ya shule kufunguliwa rasmi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi , Kisena Mabuba amesema kwamba  Halmashauri kwa kutambua juhudi na kazi kubwa iliyofanywa na Wananchi katika ujenzi wa miundombinu ya Sekondari hiyo, wameamua kuunga mkono na kushirikiana nao kwa kuwapatia mabati 108 ambayo ni bando tisa zenye thamani ya shilingi Milioni 2.8 hata hivyo wataendelea kutoa mchango na kushirikiana na Wananchi kwa kila hatua.

Amesema kwamba Halmashauri inatekeleza maagizo na maelekezo ya Mhe, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa ambaye ameagiza Wanafunzi wote watakaochaguliwa kufikia  tarehe 28 mwezi Februari  mwakani waanze masomo haraka hivyo mikakati na juhudi zinaendelea kufanyika kwa kila Kata kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa vyumba vinavyopungua na kukamilisha  ujenzi wa shule mpya ili Wanafunzi waweze kusoma.

Ameongeza kwamba Viongozi wa ngazi ya Wilaya wameamua kuungana na Wananchi wa Gambajiga kufanya kazi katika sikukuu ya Uhuru na wameshiriki pia kupanda miti katika maeneo ya Shule na kuweka vifusi katika msingi wa vyumba vya madarasa ili kutekeleza adhima ya Serikali ya  Hapa kazi tu na wtaendelea kuwashika mkono na hatimaye kukamilisha ujenzi huo hadi Wanafunzi watakapoanza masomo mwakani.

Awali akielezea namna Wananchi walivyoshiriki katika ujenzi wa vyumba 4 vya madarsa, Jengo la Utawala na ofisi ya Walimu, Choo ambavyo mbaoma yamekamilika  pamoja na kuanzisha vyumba vingine vya madarasa. Mwenyekiti wa Kijiji cha Gambajiga Jeremiah Njilima  amesema kwamba Wananchi hao waliopo kwenye Kaya 447 waliamua kuanza ujenzi huo mwezi Agosti mwaka huu 2020 kwa kuchangia mchango wa shilingi elfu 50 kila Kaya kwa awamu mbili ambapo wamefanikiwa kujenga vyumba hivyo na kufikia hatua ya boma.


Baadhi ya vyumba viwili vya Madarasa vimekamilika kwa hatua ya boma na matarajio ni kueezeka na kukamilisha tayari kwa ajil ya kufunguliwa mwezi Januari mwaka 2021 kwa Shule ya Sekondari Gambajiga Kata ya Kanyelele.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Kisena Mabuba akipanda mti katika maeneo ya Shule mpya ya Gambajiga katika Sikukuu ya Uhuru mwaka 2020.


Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Juma Sweda akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Gambajiga (walnaonekana pichani ) wakati wa kukabidhi mabati 108 kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa ya Sekondari hiyo amabyo imejengwa kwa nguvu na michango ya Wananchi.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA DARASA LA IV-2020 January 15, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI SEKRETARIETI YA AJIRA 17 JAN,2021 January 17, 2021
  • TANGANZO LA NAFASI ZA KAZI SEKRETARIETI YA AJIRA 22 JAN,2021 January 22, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI SEKRETARIETI YA AJIRA 28 JAN,2021 January 28, 2021
  • Angalia yote

Habari Mpya

  • Baraza la Madiwani lapitisha rasimu ya Bajeti ya shilingi Bilioni 44.3 mwaka 2021/2022 Misungwi.

    February 17, 2021
  • Mwanamke mwenye Ulemavu wa Miguu akabidhiwa Mkopo wa Bajaji ya Abiria Misungwi

    February 14, 2021
  • Waziri Jafo awasifu Viongozi Misungwi, kwa usimamizi mzuri ujenzi wa Hospitali Wilaya

    January 05, 2021
  • Waziri Kalemani aagiza Tannesco kuweka Transfoma Mgodi wa Busolwa na maeneo ya Usagara Misungwi

    December 31, 2020
  • Angalia yote

Video

Uzinduzi wa Tovuti za Mikoa pamoja na Halmashauri
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Takwimu za wanafunzi kitaifa
  • Taarifa
  • Kujisajili chama cha Mapinduzi-ccm
  • MFUMO WA UJAZAJI MATAMKO KWA NJIA YA MTANDAO
  • KUPATA KIUNGANISHI CHA MFUMO WA TAARIFA ZA SHULE-SIS
  • Historia ya Halmashauri
  • Sheria Mbalimbali
  • Wasiliana Nasi
  • Malalamiko

Viunganishi Linganishi

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tamisemi
  • Mwanza Region
  • Wakala wa Serikali Mtandao (Ega)

Ramani ya Wasomaji

world map hits counter

Wasomaji

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Misungwi

    Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI

    Simu ya Mezani: +255282983268

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2020 Misungwi District Council . All rights reserved.