• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Maeneo ya Vivutio vya Utalii
    • Maeneo ya Kilimo
    • Maeneo ya Madini
    • Maeneo ya Uwekezaji wa Mazingira
  • Huduma Zetu
    • Huduma Sekta ya Afya
    • Huduma Sekta ya Elimu
    • Huduma Sekta ya Maji
    • Huduma Sekta ya Mazingira
    • Huduma Sekta ya Maendeleo ya Jamii
    • Huduma Sekta ya Ardhi na Maliasili
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Huduma za Kijamii
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba Vikao vya Halmashauri
  • Miradi mbalimbali
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Mbalimbali
    • Taratibu
    • Gazeti la Serikali
    • Taarifa
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Video Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Habari Mpya

Waziri Jafo awasifu Viongozi Misungwi, kwa usimamizi mzuri ujenzi wa Hospitali Wilaya

Imewekwa : January 5th, 2021

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jaffo aridhishwa na hatua ya ujenzi  uliokamilika wa Majengo mawili ya Hospitali ya Wilaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza.

Akizungumza katika ziara yake ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi inayojengwa katika Kijiji cha Iteja na Mwamanga Waziri Jaffo amepongeza na kuwasifia Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kwa juhudi walizofanya katika kusimamia hatua zote za ujenzi wa majengo mawili ya maabara na jengo la Wagonjwa wa nje ambayo yamejengwa kwa gharama ya shilingi Milioni 488.6 hadi kukamilika kati ya fedha zilizotolewa na Serikali shilingi milioni 500.

“Kwa hiyo Mkuu wa Mkoa katika Jengo lililosimamiwa vizuri ni hili hapa , na hapa nimeridhika sana manake maeneo mengine watu wanaweka bati reject lakini hapa kila eneo ni safi na Wasukuma wenzangu hapa watafurahi sana watatamani kuumwa tu hata kama wamegombana na waume au wake zao ”. Alisisitiza Waziri Jafo

Waziri Jafo amesema kwamba jengo la Misungwi limesimamiwa vizuri sana Jengo la Misungwi katika kila eneo ukiangalia milango, vyoo hadi paa vyote ni vizuri tu, jingo ni zuri sana, nimeona hadi chooni ukimwaga maji yanatiririka na kueleza kwamba atapeleka salam kwa Mhe, Rais ili aweze kuongeza fedha za kuendelea na ujenzi na kukamilika kwa Hospitali.

Waziri Jafo ameongeza na kupongeza ushirikiano uliopo baina ya Viongozi wa Wilaya na Watendaji wa Halmashauri ambao ndio umefanikisha kazi kubwa ya ujenzi kufanyika na kuomba maeneo mengine kuiga mfano huo na kutekeleza miradi kwa kiwango na ubora mzuri unaokubalika na kuonekana.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela alishukuru sana kwa Serikali ya awamu ya tano kwa kutoa fedha za miradi mbalimbali ikwemo na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na kuahidi kuendelea kusimamia kikamilifu miradi mingine inayoendelea.

Awali akiwasilisha taarifa ya ujenzi Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt, Raymond Nyasebwa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri alieleza kwamba utekelezaji wa ujenzi huu ulianza  tarehe 11/06/2020 kwa majengo mawili yaani ujenzi wa Maabara na Jengo la wagonjwa wa nje (OPD).

Dkt. Nyasebwa amesema kuwa Halmashauri imetekeleza ujenzi huu kwa kutumia njia ya “Force account” kwa kusimamia ujenzi chini ya Wahandisi wa Halmashauri  kwa kutumia watalaamu na vifaa vyake, kuajiri mafundi/vibarua wa muda na kushirikisha Jamii,  mradi huu umenufaisha  wananchi  156 kwa kupata ajira ya muda mfupi na kuongeza kipato chao.

Alisema jumla ya shilingi milioni 488,671,134. zimetumika kununua vifaa vya ujenzi na kulipa mafundi kwa ajili ya majengo yote mawili na kubakiwa na kiasi cha shilingi milioni 11,328,866 hadi sasa utekelezaji wa mradi  kwa majengo yote mawili yaani Maabara na jengo la wagonjwa wa nje - OPD umekamilika kwa asilimia 98, aidha Halmashauri inategemea kuanza kutoa huduma mapema mwezi Februari 2021.


Mwonekano wa Jengo la Wagonjwa wa nje OPD ambalo limejengwa katika Hospitali mpya  ya Wilaya ya Misungwi.

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa,(TAMISEMI) Selemani Jafo (katikati) akikagua na kuona maeneo ya ndani ya ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje lililojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi mapema jana (Kulia ni) Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Kisena Mabuba  (Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Juma Sweda wakiwa katika ziara hiyo.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA DARASA LA IV-2020 January 15, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI SEKRETARIETI YA AJIRA 17 JAN,2021 January 17, 2021
  • TANGANZO LA NAFASI ZA KAZI SEKRETARIETI YA AJIRA 22 JAN,2021 January 22, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI SEKRETARIETI YA AJIRA 28 JAN,2021 January 28, 2021
  • Angalia yote

Habari Mpya

  • Baraza la Madiwani lapitisha rasimu ya Bajeti ya shilingi Bilioni 44.3 mwaka 2021/2022 Misungwi.

    February 17, 2021
  • Mwanamke mwenye Ulemavu wa Miguu akabidhiwa Mkopo wa Bajaji ya Abiria Misungwi

    February 14, 2021
  • Waziri Jafo awasifu Viongozi Misungwi, kwa usimamizi mzuri ujenzi wa Hospitali Wilaya

    January 05, 2021
  • Waziri Kalemani aagiza Tannesco kuweka Transfoma Mgodi wa Busolwa na maeneo ya Usagara Misungwi

    December 31, 2020
  • Angalia yote

Video

Uzinduzi wa Tovuti za Mikoa pamoja na Halmashauri
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Takwimu za wanafunzi kitaifa
  • Taarifa
  • Kujisajili chama cha Mapinduzi-ccm
  • MFUMO WA UJAZAJI MATAMKO KWA NJIA YA MTANDAO
  • KUPATA KIUNGANISHI CHA MFUMO WA TAARIFA ZA SHULE-SIS
  • Historia ya Halmashauri
  • Sheria Mbalimbali
  • Wasiliana Nasi
  • Malalamiko

Viunganishi Linganishi

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tamisemi
  • Mwanza Region
  • Wakala wa Serikali Mtandao (Ega)

Ramani ya Wasomaji

world map hits counter

Wasomaji

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Misungwi

    Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI

    Simu ya Mezani: +255282983268

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2020 Misungwi District Council . All rights reserved.