Huduma za Sekta ya Elimu Msingi
HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA IDARA YA ELIMU YA MSINGI;
Kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa taarifa za ukaguzi wa shule za msingi.
Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na miongozo ya Elimu rasmi na elimu nje ya mfumo rasmi pamoja na uboreshwaji wa Taaluma
Kuratibu na kusimamia uendeshaji wa majaribio, mitihanai ya ndani, mkoa na Taaifa Elimu ya msingi.
Kuratibu na Kusimamia ufanyikaji wa mashindano ya Taaluma kwa shule za msingi yanayoadhimishwa katika kilele cha wiki la elimu kila mwaka.
Kuratibu na kusimamia Elimu nje ya mfumo rasmi kupitia mpango wa elimu kwa walioikosa (MEMKWA)
Kusimamia na kuendesha Uwiano wa Kielimu kati ya Jamii (MUKEJA) kupitia vikundi vya ujasiriamali.
Kuratibu na Kusimamia ufanyikaji wa michezo na mashindano ya michezo ya UMITASHUMTA kwa shule za msingi.
Kusimamia na kuhakikisha walimu na watumishi wengine wasio. Walimu wa shule za msingi wanafanyiwa tathmini ya wazi ya utendaji kazi (OPRAS).
Kuratibu na kusimamia ukusanyaji, uchambuzi na utumaji/utoaji wa takwimu sahihi za Elimu ya msingi.
Kusimamia na kufuatilia ukarabati, upanuzi na ujenzi wa shule za msingi.
Kuratibu na kusimamia uagizaji na usambazaji wa vifaa vya shule kufuatana mahitaji ya shule.
Kufanya makisio ya walimu na walimu wa ufundi kulingana na idadi ya shule na Wanafunzi.
Kusimamia usajili wa shule za Serikali na zisizo za Serikali
Kukusanya takwimu, kuchambua na kuunganisha
Kushughulikia uhamisho wa ndani na nje ya Mkoa kwa wanafunzi
Kuhakikisha haki za walimu zinalipwa kwa wakati
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.