Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango yapongeza na kuridhishwa na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na kusimamiwa vizuri na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza.
Akizungumza katika ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo Novemb/9/ 2023, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe, Kashinje Machibya amepongeza Menejimenti na Watendaji kwa kusimamia kikamilifu miradi hiyo ya maendeleo ambayo imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa kwa fedha za Serikali, wafadhili na michango ya Wananchi.
Mhe, Machibya amesema kwamba kiujumla miradi imetekelezwa kwa kiwango na ubora na thamani ya fedha inaonekana ambapo katika mradi wa ujenzi wa nyumba viwili vya madarasa,ofisi ya Walimu na choo matundu sita katika Shule ya Msingi Nduha iliyopo Kata ya Kasololo ambayo imetengewa kiasi cha shilingi milioni 69,013,717 Fedha kutoka Serikali Kuu kupitia Mradi wa TASAF.
Mhe, Machibya amesema kwa ujenzia unaendelea katika Shule ya Sekondari Manawa uko katika hatua nzuri na unaridhisha ambapo walikagua ujenzi wa nyumba ya watumishi 2 in 1 ambayo iko katika hatua ya ukamilishaji na mpaka sasa imetumia shilingi milioni 70 Fedha kutoka serikali kuu kupitia mradi wa SEQUIP na inatarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Mhe, Kashinje Machibya amesema kwa ujenzia unaendelea katika Shule ya Sekondari Mwanangwa uko katika hatua nzuri na unaridhisha ambapo walitembelea na kukagua Ujenzi wa Maabara ambayo imetengewa Shilingi milioni 98,274,858.03/= na jengo la Utawala ambapo linakadiriwa kutumia Shilingi milioni 114,896,306.25/= hadi kukamilika Fedha kutoka Serikali Kuu kupitia mradi wa TASAF na kuwataka wasimamizi wa Shule hiyo waendelee kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maelekezo wanayopewa na wataalamu ili kufanya kazi nzuri na yenye viwango bora vinavyotakiwa katika ujenzi.
Ziara ya Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango pia imetembelea na kukagua miradi mingine ikiwemo mradi wa ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari mwambola iliyopo Kijiji cha Mwambola Kata ya Misungwi ambayo iko katika hatua ukamilishaji hadi kukamilika inatarajiwa kutumia Shilingi milioni 584,280,028/= ikiwa na jengo1 la utawala,madarasa 8,jengo la maktaba,jengo la Kompyuta na Maabara 3 na Vyoo matundu 8.
Vilevile Wajumbe wa Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango wameridhishwa na ujenzi wa ukamilishaji wa mabweni ya Sekondari ya Wasichana Misungwi ambapo walitembelea na kukagua hatua za ukamilishaji wa mabweni hayo na fedha iliyotengwa ni shilingi milioni 62,000,000/= na fedha ambayo imetumika mpaka sasa ni shilingi milioni 29,950,000/= kupitia mradi wa EP4R.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Misungwi Bw.Joseph Mafuru amesema kwa kushirikiana na Menejimenti ataendelea kusimamia kwa uadilifu mkubwa na kuhakikisha miradi maendeleo yote inakamilika ili wananchi waweze kupata huduma bora inayostahili kwa wakati.
Mwonekano wa nyumba ya watumishi ya 2 in 1 katika Shule ya Sekondari Manawa Misasi ambapo ipo katika hali ya ukamilishaji imejengwa kwa fedha za Serikali kuu kupitia mradi wa SEQUIP
Mwonekano wa jengo mabweni ya Wasichana katika Shule ya Sekondari Misungwi ambapo yalitengewa kiasi cha shilingi milioni 62 Fedha kutoka Serikali kuu kupitia mradi wa EP4R
Halmashauri ya Wilaya Misungwi
Sanduku la Posta: P.O Box 20 MISUNGWI
Simu ya Mezani: +255282983268
Simu ya Mkononi: 0717259106
Barua Pepe: ded@misungwidc.go.tz
Copyright ©2021 Misungwi District Council . All rights reserved.